Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 201 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ حَسَنَةٗ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ ﴾
[البَقَرَة: 201]
﴿ومنهم من يقول ربنا آتنا في الدنيا حسنة وفي الآخرة حسنة وقنا﴾ [البَقَرَة: 201]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa watu kuna kikundi chenye Imani kinachosema katika dua yake, «Mola wetu, tupe duniani afya, mali, elimu inufaishayo, vitendo vyema na mengineyo katika mambo ya dini na dunia. Na katika Akhera, tupe Pepo na utuepushie adhabu ya Moto.» Dua hii ni miongoni mwa dua zilizokusanya. Kwa hivyo, ilikuwa ni dua ambayo Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alikuwa akiiyomba mara nyingi zaidi, kama ilivyothibiti kwenye Sahihi Mbili: ya Bukhari na ya Muslim |