Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 211 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿سَلۡ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ كَمۡ ءَاتَيۡنَٰهُم مِّنۡ ءَايَةِۭ بَيِّنَةٖۗ وَمَن يُبَدِّلۡ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ﴾
[البَقَرَة: 211]
﴿سل بني إسرائيل كم آتيناهم من آية بينة ومن يبدل نعمة الله﴾ [البَقَرَة: 211]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waulize, ewe Mtume, Wana wa Isrāīl wanaokufanyia ukaidi, «Ni aya ngapi zilizo wazi tulizowapa katika vitabu vyao zinazowaongoza wao njia ya haki, wakazikanusha,wakazipa nyongo na wakazipotosha kwa kuzitoa kwenye malengo yake.» Na atakayebadisha neema ya Mwenyezi Mungu, nayo ni dini Yake, na akaikanusha baada ya kuijua na hoja yake kumsimamia, basi Mwenyezi Mungu ni Mkali wa mateso kwake |