Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 212 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَيَسۡخَرُونَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۘ وَٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ وَٱللَّهُ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ ﴾
[البَقَرَة: 212]
﴿زين للذين كفروا الحياة الدنيا ويسخرون من الذين آمنوا والذين اتقوا فوقهم﴾ [البَقَرَة: 212]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wale walioukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu wamepambiwa maisha ya dunia na vilivyomo humo vya matamanio na vilivyo tamu, na huku wao wanawafanyia shere Waumini. Na hawa wanaomcha Mola wao watakuwa juu ya Makafiri wote Siku ya Kiyama, ambapo Mwenyezi Mungu Atawatia katika Pepo ya daraja za juu na Atawateramsha Makafiri ndani ya mashimo ya Moto ya chini. Mwenyezi Mungu Anamruzuku Amtakaye, katika viumbe vyake, bila ya hesabu |