Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 210 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن يَأۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ فِي ظُلَلٖ مِّنَ ٱلۡغَمَامِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ ﴾
[البَقَرَة: 210]
﴿هل ينظرون إلا أن يأتيهم الله في ظلل من الغمام والملائكة وقضي﴾ [البَقَرَة: 210]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hawangojei hawa wakaidi wenye kukanusha, baada ya kusimama dalili wazi, isipokuwa Awajie Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, kwa namna inayolingana na Yeye, Aliyetakasika na kila sifa mbaya, katika vivuli vya Mawingu Siku ya Kiyama ili Aamue baina yao kwa hukumu adilifu, na waje Malaika. Wakati huo, Atahukumu Mwenyezi Mungu, kati yao, hukumu Yake. Na kwake Yeye Peke Yake hurudishwa mambo yote ya viumbe |