×

Wala si vibaya kwenu katika kupeleka posa kwa ishara tu kwa wanawake 2:235 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:235) ayat 235 in Swahili

2:235 Surah Al-Baqarah ayat 235 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 235 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا عَرَّضۡتُم بِهِۦ مِنۡ خِطۡبَةِ ٱلنِّسَآءِ أَوۡ أَكۡنَنتُمۡ فِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمۡ سَتَذۡكُرُونَهُنَّ وَلَٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّآ أَن تَقُولُواْ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗاۚ وَلَا تَعۡزِمُواْ عُقۡدَةَ ٱلنِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ ٱلۡكِتَٰبُ أَجَلَهُۥۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 235]

Wala si vibaya kwenu katika kupeleka posa kwa ishara tu kwa wanawake waliomo edani au mkadhamiria katika nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msiwaahidi kwa siri, ila mnene maneno mema. Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka eda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo katika nafsi zenu. Basi tahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ولا جناح عليكم فيما عرضتم به من خطبة النساء أو أكننتم في, باللغة السواحيلية

﴿ولا جناح عليكم فيما عرضتم به من خطبة النساء أو أكننتم في﴾ [البَقَرَة: 235]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na wala nyinyi hamna dhambi, enyi wanaume, katika ishara mnazozitoa za kutaka kuwaoa wanawake waliofiliwa na waume zao au wale waliopewa talaka ya mwisho, wakiwa wako katika eda lao. Pia hamna dhambi katika mawazo yanayowapitia ndani ya nafsi zenu ya kutaka kuwaoa wamalizapo eda lao. Mwenyezi Mungu Anajua kwamba nyinyi mtawataja wanawake walio kwenye eda na hamtasubiri kuweza kunyamaza kutowataja, kwa udhaifu wenu. Kwa ajili hiyo, Mwenyezi Mungu amewahalalishia kuwataja kwa ishara au kwa kudhamiria ndani ya nafsi zenu. Na jihadharini kuagana nao kisiri, kwa kuzini, au kukubaliana kuoana wakiwa bado wako kwenye eda, isipokuwa mtakaposema neno lenye maana kwamba mfano wake, mwanamke huyo, waume huwa wanampendelea. Wala msikusudie kufunga ndoa katika kipindi cha eda mpaka muda wake umalizike. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu Anayajua yaliyomo katika nafsi zenu, kwa hivyo muogopeni Yeye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe kwa mwenye kutubia dhambi zake, ni Mpole kwa waja Wake, Hana haraka ya kuwatesa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek