Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 234 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنكُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٰجٗا يَتَرَبَّصۡنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرۡبَعَةَ أَشۡهُرٖ وَعَشۡرٗاۖ فَإِذَا بَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا فَعَلۡنَ فِيٓ أَنفُسِهِنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ ﴾
[البَقَرَة: 234]
﴿والذين يتوفون منكم ويذرون أزواجا يتربصن بأنفسهن أربعة أشهر وعشرا فإذا بلغن﴾ [البَقَرَة: 234]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale wanaofariki kati yenu wakawaacha wake zao baada ya kufa kwao, italazimu wakae eda muda wa miezi minne na siku kumi, wasitoke majumbani mwao, wasijipambe wala wasiolewe. Na pindi muda huo uliotajwa uishapo, si dhambi kwenu, enyi mawalii wa wanawake, kwa yale watakayo kujifanyia nafsi zao, ya kutoka, kujipamba na kuolewa kwa njia iliyowekwa na Sheria. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kutakasika na kila sifa mbaya, ni Mtambuzi wa vitendo vyenu vya wazi na viliyofichika, na Atawalipa kwavyo |