Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 245 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿مَّن ذَا ٱلَّذِي يُقۡرِضُ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا فَيُضَٰعِفَهُۥ لَهُۥٓ أَضۡعَافٗا كَثِيرَةٗۚ وَٱللَّهُ يَقۡبِضُ وَيَبۡصُۜطُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ﴾
[البَقَرَة: 245]
﴿من ذا الذي يقرض الله قرضا حسنا فيضاعفه له أضعافا كثيرة والله﴾ [البَقَرَة: 245]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ni yupi ambaye atatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, kutoa kuliko kuzuri kwa kutarajia malipo, Mwenyezi Mungu Apate kumuongezea nyongeza nyingi zisizohesabika za thawabu na malipo mema? Hakika Mwenyezi Mungu Anazuia na Anatoa. Kwa hivyo, toeni wala msijali, kwani Yeye Ndiye Mruzuku, Anambana Anayemtaka, miongoni mwa waja Wake, katika riziki na Anaikunjua, hiyo riziki, kwa wengine. Ana hekima kubwa katika hayo. Na Kwake Yeye Peke Yake mtarudi baada ya kufa, na hapo Atawalipa kwa vitendo vyenu |