×

Hukuwaona watukufu katika Wana wa Israili baada ya Musa, walipo mwambia Nabii 2:246 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:246) ayat 246 in Swahili

2:246 Surah Al-Baqarah ayat 246 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 246 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ مِنۢ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ مِنۢ بَعۡدِ مُوسَىٰٓ إِذۡ قَالُواْ لِنَبِيّٖ لَّهُمُ ٱبۡعَثۡ لَنَا مَلِكٗا نُّقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ قَالَ هَلۡ عَسَيۡتُمۡ إِن كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِتَالُ أَلَّا تُقَٰتِلُواْۖ قَالُواْ وَمَا لَنَآ أَلَّا نُقَٰتِلَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَدۡ أُخۡرِجۡنَا مِن دِيَٰرِنَا وَأَبۡنَآئِنَاۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقِتَالُ تَوَلَّوۡاْ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[البَقَرَة: 246]

Hukuwaona watukufu katika Wana wa Israili baada ya Musa, walipo mwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ili tupigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: Je, haielekei ikiwa mtaandikiwa vita kuwa msipigane? Wakasema: Itakuwaje tusipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali tumetolewa majumbani kwetu na watoto wetu? Lakini walipo andikiwa kupigana waligeuka, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ألم تر إلى الملإ من بني إسرائيل من بعد موسى إذ قالوا, باللغة السواحيلية

﴿ألم تر إلى الملإ من بني إسرائيل من بعد موسى إذ قالوا﴾ [البَقَرَة: 246]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwani hukukijua, ewe Mtume, kisa cha watukufu na mabwana, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, baada ya zama za Musa kupita? Walipomtaka Mtume wao amtawalishe kwao mfalme, wapate kukusanyika chini ya uongozi wake na wapate kupigana na maadui zao katika njia ya Mwenyezi Mungu. Nabii wao akawaambia, «Je, mambo ni kama vile ninavyoyatarajia kwamba lau mtafaradhiwa kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa hamtapigana? Kwani mimi nachelea mtaogopa na mtakimbia vitani.» Wakasema wakikanusha matarajio ya Nabii wao, «Ni kizuizi kipi kitakacho kutuzuia tusipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu, ambapo adui yetu ametutoa kwenye Makao yetu na akatutenganisha na na watoto wetu kwa kutuua na kututeka?» Basi Mwenyezi Mungu Alipowafaradhia kupigana wakiwa na mfalme Aliyewachagulia walikuwa waoga na wakakimbia vitani, isipokuwa wachache kati yao waliojikita imara kwa fadhila za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Anawajua mno madhalimu, wenye kuzivunja ahadi zao
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek