×

MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao 2:253 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:253) ayat 253 in Swahili

2:253 Surah Al-Baqarah ayat 253 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 253 - البَقَرَة - Page - Juz 3

﴿۞ تِلۡكَ ٱلرُّسُلُ فَضَّلۡنَا بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۘ مِّنۡهُم مَّن كَلَّمَ ٱللَّهُۖ وَرَفَعَ بَعۡضَهُمۡ دَرَجَٰتٖۚ وَءَاتَيۡنَا عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدۡنَٰهُ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِۗ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلَ ٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ وَلَٰكِنِ ٱخۡتَلَفُواْ فَمِنۡهُم مَّنۡ ءَامَنَ وَمِنۡهُم مَّن كَفَرَۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلُواْ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَفۡعَلُ مَا يُرِيدُ ﴾
[البَقَرَة: 253]

MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isa mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio amini, na wengine kati yao walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo

❮ Previous Next ❯

ترجمة: تلك الرسل فضلنا بعضهم على بعض منهم من كلم الله ورفع بعضهم, باللغة السواحيلية

﴿تلك الرسل فضلنا بعضهم على بعض منهم من كلم الله ورفع بعضهم﴾ [البَقَرَة: 253]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mitume hawa watukufu, Mwenyezi Mungu Amewatukuza baadhi yao juu ya wengine, kulingana na neema za Mwenyezi Mungu juu yao. Miongoni mwao kuna ambao Mwenyezi Mungu Amesema nao, kama Mūsā na Muhammad, rehema na amani ziwashukie. Katika hili pana kuthibitisha sifa ya kusema kwa Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake. Na miongoni mwao kuna ambao Mwenyezi Mungu Aliwainua daraja nyingi za juu, kama Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kuenea ujumbe wake, kutia kikomo cha unabii kwake, kwa kuwatukuza ummah wake juu ya ummah wengine na yasiyokuwa hayo. Na Mwenyezi Mungu Alimpa 'Īsā mwana wa Maryam, amani imshukie, hoja zilizo wazi, ambazo ni miujiza yenye kushinda, kama kumponya aliyezaliwa kipofu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na kumponya mwenye barasi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kama kuhuisha kwake waliokufa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Alimpa nguvu kwa Jibrili, amani imshukie. Na lau Mwenyezi Mungu Alitaka wasipigane hao waliokuja baada ya hawa Mitume, baada ya kuwafunukia wao hoja zilizo wazi, hawangalipigana. Lakini ilitokea tafauti baina yao: katika wao kuna aliyejikita kwenye Imani yake, na katika wao kuna aliyeshikilia kukanusha. Na lau Mwenyezi Mungu Alitaka, baada ya hizo tafauti zilizotokea zilizopelekea kupigana, hawangalipigana, lakini Mwenyezi Mungu Anampa taufik ya kumtii Yeye na kumuamini Anayemtaka, na Anamuondolea taufiki Yake Anayemtaka akamuasi na kumkanusha, Kwani Yeye Anafanya na kuchagua Analolitaka
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek