×

Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye 2:256 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:256) ayat 256 in Swahili

2:256 Surah Al-Baqarah ayat 256 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 256 - البَقَرَة - Page - Juz 3

﴿لَآ إِكۡرَاهَ فِي ٱلدِّينِۖ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشۡدُ مِنَ ٱلۡغَيِّۚ فَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلطَّٰغُوتِ وَيُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسۡتَمۡسَكَ بِٱلۡعُرۡوَةِ ٱلۡوُثۡقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَاۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴾
[البَقَرَة: 256]

Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua

❮ Previous Next ❯

ترجمة: لا إكراه في الدين قد تبين الرشد من الغي فمن يكفر بالطاغوت, باللغة السواحيلية

﴿لا إكراه في الدين قد تبين الرشد من الغي فمن يكفر بالطاغوت﴾ [البَقَرَة: 256]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwa kuwa Dini hii imekamilika na hoja zake ziko wazi, haihitajii ilazimishwe kwa watu ambao jizya (jizyah) inapokewa kutoka kwao. Kwani dalili ziko wazi ambazo kwa dalili hizo inabainika haki, ikawa kando na batili, na uongofu, ukawa kando na upotevu. Basi mwenye kukanusha vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu na akamuamini Mwenyezi Mungu, huwa amethibiti na kulingana kwenye njia bora na ameshikamana na kamba imara ya Dini isiyokatika. Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa maneno ya waja Wake, ni Mjuzi wa nia zao na vitendo vyao na Atawalipa kwa hayo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek