×

Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio 2:26 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:26) ayat 26 in Swahili

2:26 Surah Al-Baqarah ayat 26 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 26 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿۞ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسۡتَحۡيِۦٓ أَن يَضۡرِبَ مَثَلٗا مَّا بَعُوضَةٗ فَمَا فَوۡقَهَاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۘ يُضِلُّ بِهِۦ كَثِيرٗا وَيَهۡدِي بِهِۦ كَثِيرٗاۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِۦٓ إِلَّا ٱلۡفَٰسِقِينَ ﴾
[البَقَرَة: 26]

Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walio amini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, lakini wale walio kufuru husema: Ni nini analo kusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini hawapotezi ila wale wapotovu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن الله لا يستحيي أن يضرب مثلا ما بعوضة فما فوقها فأما, باللغة السواحيلية

﴿إن الله لا يستحيي أن يضرب مثلا ما بعوضة فما فوقها فأما﴾ [البَقَرَة: 26]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Halionei haya jambo la haki lolote kulitaja, liwe ni kubwa au dogo, hata kama ni kukipigia mfano kitu kidogo sana, kama mbu na nzi na mfano wake, katika vitu Alivyovipigia mfano Mwenyezi Mungu kuonyesha kushindwa kwa kila kitu kinachoabudiwa kisichokuwa Mwenyezi Mungu. Ama waumini, wao wanajua hekima ya Mwenyezi Mungu katika kupigia mfano kitu kikubwa au kidogo miongoni mwa viumbe Vyake. Ama makafiri, wanafanya maskhara na kusema, “Ni nini lengo la Mwenyezi Mungu kupigia mfano vidudu hivi vitwevu?” Mwenyezi Mungu anawajibu kwamba makusudio ni kuwafanyia mtihani na kupambanua Mwenye Imani na kafiri. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu, kwa mifano hii, anawaepusha na haki watu wengi, kwa kuifanyia kwao maskhara, na Anawapa taufiki kwayo wengineo kupata nyongeza ya Imani na uongofu. Na Mwenyezi Mungu Hamdhulumu yeyote, kwani Hawaepushi na haki isipokuwa wenye kutoka nje ya utiifu Kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek