Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 264 - البَقَرَة - Page - Juz 3
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُبۡطِلُواْ صَدَقَٰتِكُم بِٱلۡمَنِّ وَٱلۡأَذَىٰ كَٱلَّذِي يُنفِقُ مَالَهُۥ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۖ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ صَفۡوَانٍ عَلَيۡهِ تُرَابٞ فَأَصَابَهُۥ وَابِلٞ فَتَرَكَهُۥ صَلۡدٗاۖ لَّا يَقۡدِرُونَ عَلَىٰ شَيۡءٖ مِّمَّا كَسَبُواْۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ ﴾
[البَقَرَة: 264]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا تبطلوا صدقاتكم بالمن والأذى كالذي ينفق ماله رئاء﴾ [البَقَرَة: 264]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, msiziondoe thawabu za vitu vile mlivyovitoa sadaka kwa usumbulizi na kero. Kwani huyu, mwenye kufanya haya, anafanana na mtu atowaye mali yake ili watu wamuone na wamsifu ilhali yeye hamuamini Mwenyezi Mungu wala hana yakini na Siku ya Akhera. Mfano wa huyo ni mfano wa jiwe laini lenye mchanga juu yake, lililonyeshewa na mvua nyingi, ikaondoa ule mchanga, ikaliacha tupu halina kitu juu yake. Basi hawa wenye kufanya ria ndivo walivyo, amali zao zinapotea mbele ya Mwenyezi Mungu na hawapati chochote cha thawabu kwa utoaji wao. Na Mwenyezi Mungu hawaafikii makafiri kuifikia haki katika vitu wanvyovitoa na mengineyo |