Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 283 - البَقَرَة - Page - Juz 3
﴿۞ وَإِن كُنتُمۡ عَلَىٰ سَفَرٖ وَلَمۡ تَجِدُواْ كَاتِبٗا فَرِهَٰنٞ مَّقۡبُوضَةٞۖ فَإِنۡ أَمِنَ بَعۡضُكُم بَعۡضٗا فَلۡيُؤَدِّ ٱلَّذِي ٱؤۡتُمِنَ أَمَٰنَتَهُۥ وَلۡيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥۗ وَلَا تَكۡتُمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَۚ وَمَن يَكۡتُمۡهَا فَإِنَّهُۥٓ ءَاثِمٞ قَلۡبُهُۥۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 283]
﴿وإن كنتم على سفر ولم تجدوا كاتبا فرهان مقبوضة فإن أمن بعضكم﴾ [البَقَرَة: 283]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mkiwa muko safarini, na msipate mwenye kuwaandikia, mpatieni yule mwenye haki kitu kiwe ni dhamana ya haki yake hadi mdaiwa atakapolipa deni yake. Na iwapo nyinyi kwa nyinyi mumeaminiana, hapana makosa kuacha kuandika, kushuhudisha na kuweka rahani, na deni itabaki ni amana kwenye shingo ya mdaiwa, ni juu yake kuilipa. Na ni juu yake amchunge Mwenyezi Mungu asimfanyiye hiana mwenzake. Na akikataa mdaiwa deni iliyo juu yake, na ikawa pana mtu aliyekuweko na kushuhudia, huyo itamlazimu kuutoa wazi ushahidi wake. Na mwenye kuuficha ushahudi huu, ni mtu mwenye moyo wa hiana na urongo. Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuchungulia siri zote, Ndiye Ambaye ujuzi Wake umezunguka mambo yenu yote, na Atawahesabu kwa hayo |