×

Viliomo mbinguni na viliomo duniani ni vya Mwenyezi Mungu. Na mkidhihirisha yaliyomo 2:284 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:284) ayat 284 in Swahili

2:284 Surah Al-Baqarah ayat 284 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 284 - البَقَرَة - Page - Juz 3

﴿لِّلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَإِن تُبۡدُواْ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ أَوۡ تُخۡفُوهُ يُحَاسِبۡكُم بِهِ ٱللَّهُۖ فَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ ﴾
[البَقَرَة: 284]

Viliomo mbinguni na viliomo duniani ni vya Mwenyezi Mungu. Na mkidhihirisha yaliyomo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atakuhisabuni kwayo. Kisha amsamehe amtakaye na amuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: لله ما في السموات وما في الأرض وإن تبدوا ما في أنفسكم, باللغة السواحيلية

﴿لله ما في السموات وما في الأرض وإن تبدوا ما في أنفسكم﴾ [البَقَرَة: 284]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, kwa kuvimiliki, kuvipekesha na kuvijua. Hakuna chochote kinachofichika Kwake. Na chochote mnachokidhihirisha, kati ya viliomo ndani ya nafsi zenu au mnachokificha, Mwenyezi Mungu Anakijua, na Atawahesabu nacho. Atamsamehe Anayemtaka na Atampatiliza Anayemtaka. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu. Baadaye Mwenyezi Mungu aliwakirimu Waislamu Akasamehe maneno ya mtu kuiyambia nafsi yake na mawazo ya moyo, yakiwa hayatafuatiwa na maneno au vitendo, kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek