Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 57 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَظَلَّلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡغَمَامَ وَأَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰۖ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ ﴾
[البَقَرَة: 57]
﴿وظللنا عليكم الغمام وأنـزلنا عليكم المن والسلوى كلوا من طيبات ما رزقناكم﴾ [البَقَرَة: 57]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Kumbukeni neema Zetu mlipokuwa mnahangaika kwenye ardhi, tukawaletea kiwingu cha kuwafinika ili kiwakinge na joto la jua, tukawateremshia mann, nacho ni ktu kifananacho na gundi chenye ladha ya asali; na tukawateremshia salwa, nayo ni aina ya ndege wafananao na tomboro; na tukawaambia, “Kuleni vitu vizuri tulivyowaruzuku na msiende kinyume na dini ya Mwenyezi Mungu,” lakini hamkufuata amri. Na wao hawakutudhulumu sisi kwa kuzikanusha neema hizi, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao, Kwani mwisho mbaya wa dhuluma utawarudia wao |