Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 60 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿۞ وَإِذِ ٱسۡتَسۡقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ فَقُلۡنَا ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡحَجَرَۖ فَٱنفَجَرَتۡ مِنۡهُ ٱثۡنَتَا عَشۡرَةَ عَيۡنٗاۖ قَدۡ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٖ مَّشۡرَبَهُمۡۖ كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ مِن رِّزۡقِ ٱللَّهِ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ ﴾
[البَقَرَة: 60]
﴿وإذ استسقى موسى لقومه فقلنا اضرب بعصاك الحجر فانفجرت منه اثنتا عشرة﴾ [البَقَرَة: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Kumbukeni neema Yetu kwenu, mlipokuwa na kiu katika kuzunguka kwenu, alipotuomba Musa, kwa unyenyekevu, tuwaletee maji watu wake. Tukasema, “Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako.” Akalipiga, na chemchemi zikabubujika hapo jiweni sehemu kumi na mbili, ikilingana na idadi ya makabila yao, pamoja na kulijulisha kila kabila chemchemi yake ya kutumia, ili wasigombane. Na tukawaambia, “Kuleni na kunyweni riziki ya Mwenyezi Mungu wala msitembee katika ardhi kuleta uharibifu.” |