×

Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini 2:62 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:62) ayat 62 in Swahili

2:62 Surah Al-Baqarah ayat 62 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 62 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلنَّصَٰرَىٰ وَٱلصَّٰبِـِٔينَ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَلَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ﴾
[البَقَرَة: 62]

Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن الذين آمنوا والذين هادوا والنصارى والصابئين من آمن بالله واليوم الآخر, باللغة السواحيلية

﴿إن الذين آمنوا والذين هادوا والنصارى والصابئين من آمن بالله واليوم الآخر﴾ [البَقَرَة: 62]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika Waumini wa ummah huu waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake na wakatekeleza Sheria Yake, na wale waliokuwa kabla ya kutumilizwa Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, miongoni mwa ummah waliopita katika Mayahudi, Wanaswara na Wasabai (Sābiūn), nao ni watu walioko kwenye tabia za maumbile na hawana dini maalumu wanayoifuata, wote hawa wakimuamini Mwenyezi Mungu, imani ya sawa iliyotakasika, wakaiamini Siku ya kufufuliwa na Malipo na wakafanya amali zenye kumridhi Mwenyezi Mungu, basi thawabu zao zimethibiti kwa Mola wao. Wao hawatakuwa na khofu juu ya mambo yao ya Akhera ambayo wao watayakabili. Na wala wao hawatahuzunika juu ya mambo ya dunia waliyoyakosa. Ama baada ya kutumilizwa Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, kuwa ni mwisho wa Manabii na Mitume, kwa watu wote, Mwenyezi Mungu Hatakubali dini, kwa yoyote, isipokuwa ile aliyokuja nayo ambayo ni Uislamu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek