Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 9 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَمَا يَخۡدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 9]
﴿يخادعون الله والذين آمنوا وما يخدعون إلا أنفسهم وما يشعرون﴾ [البَقَرَة: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wanaitakidi, kwa ujinga wao, kuwa wao wanamdanganya Mwenyezi Mungu na Waumini, kwa kudhihirisha kwao Imani na kuficha kwao ukafiri, na wao hawamdanganyi yoyote isipokuwa nafsi zao wenyewe, kwa kuwa madhara ya kudanganya kwao yanawarudia wao. Na kwa kuwa ujinga wao umekolea na nyoyo zao zimeharibika, huwa hawana hisia ya hilo |