Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 8 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَمَا هُم بِمُؤۡمِنِينَ ﴾
[البَقَرَة: 8]
﴿ومن الناس من يقول آمنا بالله وباليوم الآخر وما هم بمؤمنين﴾ [البَقَرَة: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Miongoni mwa watu kuna kundi linalokuwa katika hali ya kutokuwa na uamuzi, linasimama baina ya Waumini na makafiri, nao ni wanafiki wanaosema kwa ndimi zao, “Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho,’ na hali wao, katika undani yao, ni warongo, hawakuamini |