Quran with Swahili translation - Surah Ta-Ha ayat 72 - طه - Page - Juz 16
﴿قَالُواْ لَن نُّؤۡثِرَكَ عَلَىٰ مَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلَّذِي فَطَرَنَاۖ فَٱقۡضِ مَآ أَنتَ قَاضٍۖ إِنَّمَا تَقۡضِي هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَآ ﴾
[طه: 72]
﴿قالوا لن نؤثرك على ما جاءنا من البينات والذي فطرنا فاقض ما﴾ [طه: 72]
Abdullah Muhammad Abu Bakr wachawi wakasema kumwambia Fir'awn,« Hatutakutanguliza wewe tukakusikiliza na tukaifuata dini yako juu ya yale aliyotuletea Mūsā yaliyo waziwazi yanayojulisha ukweli wake na ulazima wa kumfuata na kumtii Mola wake. Na hatutautanguliza uola wako wa kujipangia juu ya uola wa Mwenyezi Mungu Aliyetuumba. Basi fanya kile utakachotufanya. Ukweli ni kwamba utawala wako ni hapa katika maisha ya duniani. Na utakachokifanya kwetu si kitu isipokuwa ni adhabu itakayokoma kwa kukoma dunia hii |