Quran with Swahili translation - Surah Al-Anbiya’ ayat 24 - الأنبيَاء - Page - Juz 17
﴿أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةٗۖ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡۖ هَٰذَا ذِكۡرُ مَن مَّعِيَ وَذِكۡرُ مَن قَبۡلِيۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ٱلۡحَقَّۖ فَهُم مُّعۡرِضُونَ ﴾
[الأنبيَاء: 24]
﴿أم اتخذوا من دونه آلهة قل هاتوا برهانكم هذا ذكر من معي﴾ [الأنبيَاء: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, hawa washirikina waliwafanya wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni waungu wanaonufaisha na kudhuru na wanaohuisha na kufisha? Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Leteni dalili zenu mlizonazo juu ya hao mliowafanya waungu.» Kwani hakuna, ndani ya Qur’ani niliyokuja nayo wala ndani ya Vitabu vilivyotangulia, dalili yoyote ya yale mliyoyafuata.» Na wao hawakushirikisha isipokuwa ni kwa sababu ya ujinga wao na kuigiza, kwa hivyo wao ni wenye kuupa mgongo ukweli na ni wenye kuukataa |