Quran with Swahili translation - Surah Al-Anbiya’ ayat 30 - الأنبيَاء - Page - Juz 17
﴿أَوَلَمۡ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ كَانَتَا رَتۡقٗا فَفَتَقۡنَٰهُمَاۖ وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَيۡءٍ حَيٍّۚ أَفَلَا يُؤۡمِنُونَ ﴾
[الأنبيَاء: 30]
﴿أو لم ير الذين كفروا أن السموات والأرض كانتا رتقا ففتقناهما وجعلنا﴾ [الأنبيَاء: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hawakujua hawa ambao wamekufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeshikana, hakuna kipambanuzi baina yao, hakuna mvua kutoka juu wala mimea kutoka kwenye ardhi, kisha tukazipambanua kwa uweza wetu, tukateremsha mvua kutoka juu na tukatoa mimea kutoka kwenye ardhi na tukajaalia kutokana na maji kila kitu chenye uhai. Basi je hawaamini hawa wakanushaji, wakayasadiki wanayoyaona na wakamuhusuMwenyezi Mungu tu kwa ibada |