Quran with Swahili translation - Surah Al-Anbiya’ ayat 78 - الأنبيَاء - Page - Juz 17
﴿وَدَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ إِذۡ يَحۡكُمَانِ فِي ٱلۡحَرۡثِ إِذۡ نَفَشَتۡ فِيهِ غَنَمُ ٱلۡقَوۡمِ وَكُنَّا لِحُكۡمِهِمۡ شَٰهِدِينَ ﴾
[الأنبيَاء: 78]
﴿وداود وسليمان إذ يحكمان في الحرث إذ نفشت فيه غنم القوم وكنا﴾ [الأنبيَاء: 78]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka Nabii wa Mwenyezi Mungu Dāwūd na mwane Sulaiman, ewe Mtume, walipotoa uamuzi juu ya kesi iliyoletwa na wagonvi wawili, kondoo wa mmoja wao waliharibu mimea ya mwingine, walienea kwenye mimea hiyo kipindi cha usiku wakaiharibu. Dāwūd alitoa uamuzi kwamba wale kondoo wawe ni milki ya mwenye mimea wakiwa ni badala ya mimea yake iliyoharibiwa, kwa kuwa thamani ya viwili hivyo ni sawa. Na sisi tuliushuhudia uamuzi wao, haukufichamana kwetu |