Quran with Swahili translation - Surah Al-Anbiya’ ayat 83 - الأنبيَاء - Page - Juz 17
﴿۞ وَأَيُّوبَ إِذۡ نَادَىٰ رَبَّهُۥٓ أَنِّي مَسَّنِيَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ ﴾
[الأنبيَاء: 83]
﴿وأيوب إذ نادى ربه أني مسني الضر وأنت أرحم الراحمين﴾ [الأنبيَاء: 83]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Mtume, mja wetu Ayyūb, tulipomtahini kwa madhara na ugonjwa mkubwa mwilini mwake, na akakosa watu wake, mali yake na watoto wake, akasubiri kwa kutaka thawabu, na akamlingania Mola wake, Aliyetukuka na kushinda, kwa kumuomba, «Mimi nimepatikana na madhara, na wewe Ndiye Mwenye huruma kuliko wenye huruma, basi niepushie nayo!» |