Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 16 - الحج - Page - Juz 17
﴿وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَٰهُ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖ وَأَنَّ ٱللَّهَ يَهۡدِي مَن يُرِيدُ ﴾
[الحج: 16]
﴿وكذلك أنـزلناه آيات بينات وأن الله يهدي من يريد﴾ [الحج: 16]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kama Alivyosimamisha Mwenyezi Mungu hoja, miongoni mwa dalili za uweza Wake, juu ya makafiri kuhusu ufufuzi, vilevile Aliiteremsha Qur’ani, ambayo aya zake ziko wazi katika matamshi yake na maana yake na ambayo kwayo Mwenyezi Mungu Anamuongoza anayemtaka aongoke. Kwani hakuna Mwenye kuongoa isipokuwa Yeye |