Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 15 - الحج - Page - Juz 17
﴿مَن كَانَ يَظُنُّ أَن لَّن يَنصُرَهُ ٱللَّهُ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ فَلۡيَمۡدُدۡ بِسَبَبٍ إِلَى ٱلسَّمَآءِ ثُمَّ لۡيَقۡطَعۡ فَلۡيَنظُرۡ هَلۡ يُذۡهِبَنَّ كَيۡدُهُۥ مَا يَغِيظُ ﴾
[الحج: 15]
﴿من كان يظن أن لن ينصره الله في الدنيا والآخرة فليمدد بسبب﴾ [الحج: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yoyote yule anayeitakidi kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka hatamsaidia Mtume Wake kwa kumpa ushindi ulimwenguni kwa kuipa nguvu Dini yake na huko Akhera kumtukuza daraja yake na kumuadhibu aliyemkanusha, basi anyoshe kamba aifunge kwenye sakafu ya nyumba yake kisha ajitie kitanzi kisha aikate hiyo kamba, kisha aangalie iwapo hilo litamuondolea hasira alizonazo ndani ya nafsi yake. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumnusuru Nabii Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, hapana budi |