Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 17 - الحج - Page - Juz 17
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلصَّٰبِـِٔينَ وَٱلنَّصَٰرَىٰ وَٱلۡمَجُوسَ وَٱلَّذِينَ أَشۡرَكُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ يَفۡصِلُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ ﴾
[الحج: 17]
﴿إن الذين آمنوا والذين هادوا والصابئين والنصارى والمجوس والذين أشركوا إن الله﴾ [الحج: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wale waliomumini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na Mayahudi na Sābiūn (watu waliobaki kwenye maumbile yao na hawana dini wanayoifuata) na Wanaswara na Majūs (wnaoabudu moto) na wale walioashirikisha (wanaoabudu masanamu), Mwenyezi Mungu Atapambanua baina yao wote, Siku ya Kiyama, Awatie Waumini Peponi na Awatie makafiri Motoni, Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni Shahidi, Anayashuhudia matendo yote ya waja, Anayadhibiti na Anayahifadhi, Na Atamlipa kila mtu kile anachostahili, malipo yanayolingana na matendo waliokuwa wakiyafanya |