Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 75 - الحج - Page - Juz 17
﴿ٱللَّهُ يَصۡطَفِي مِنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ رُسُلٗا وَمِنَ ٱلنَّاسِۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعُۢ بَصِيرٞ ﴾
[الحج: 75]
﴿الله يصطفي من الملائكة رسلا ومن الناس إن الله سميع بصير﴾ [الحج: 75]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anateua, miongoni mwa Malaika, wajumbe kuwatuma kwa Manabii Wake, na Anateua kutokana na watu, wajumbe wakufikisha jumbe Zake kwa viumbe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maneno ya waja Wake, Mwenye kuviona vitu vyote na yule anayemteua kwa utume miongoni mwa viumbe Wake. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake |