×

Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi 22:78 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hajj ⮕ (22:78) ayat 78 in Swahili

22:78 Surah Al-hajj ayat 78 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 78 - الحج - Page - Juz 17

﴿وَجَٰهِدُواْ فِي ٱللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِۦۚ هُوَ ٱجۡتَبَىٰكُمۡ وَمَا جَعَلَ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلدِّينِ مِنۡ حَرَجٖۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمۡ إِبۡرَٰهِيمَۚ هُوَ سَمَّىٰكُمُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ مِن قَبۡلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ ٱلرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيۡكُمۡ وَتَكُونُواْ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِۚ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱعۡتَصِمُواْ بِٱللَّهِ هُوَ مَوۡلَىٰكُمۡۖ فَنِعۡمَ ٱلۡمَوۡلَىٰ وَنِعۡمَ ٱلنَّصِيرُ ﴾
[الحج: 78]

Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وجاهدوا في الله حق جهاده هو اجتباكم وما جعل عليكم في الدين, باللغة السواحيلية

﴿وجاهدوا في الله حق جهاده هو اجتباكم وما جعل عليكم في الدين﴾ [الحج: 78]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
na zipigeni jihadi nafsi zenu, na simameni, kisimamo kikamilifu, kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na waiteni viumbe kwenye njia Yake, na piganeni jihadi kwa mali zenu, ndimi zenu na nafsi zenu, hali ya kumtakasia nia Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, kwa hayo, hali ya kuzisalimisha Kwake nyoyo zenu na viungo vyenu. Yeye Amewateua muibebe hii Dini. Na Amewapa neema kwa kuifanya Sheria Yake kuwa sahali, haina dhiki wala mikazo katika Amri zake na hukumu zake kama vile ilivyokuwa kwa baadhi ya ummah kabla yenu. Mila hii yenye usahali ndio Mila ya baba yenu Ibrāhīm. Na Mwenyezi Mungu Amewaita nyinyi Waislamu tangu nyuma kwenye Vitabu vilivyoteremshwa vilivyotangulia na katika hii Qur’ani. Na Amewahusu nyinyi kwa chaguo hili, ili mwisho wa Mitume, Mhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, awe shahidi wenu kuwa amewafikishia ujumbe wa Mola wake, na ili muwe ni mashahidi wa ummah wengine kuwa Mitume wao waliwafikishia kwa habari mlizopewa na Mwenyezi Mungu katika Kitabu Chake. Basi jibidiisheni kujua thamani ya neema hii mupate kuishukuru, na mujilazimishe kufuata maamrisho ya Dini ya Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza Swala kwa nguzo zake na sheruti zake na kutoa Zaka za faradhi, na muingie kwenye himaya ya Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, na mumtegemee Yeye, kwani yeye Ndiye Mbora wa kutegemewa kwa mwenye kumtegemea na ni Mbora wa kunusuru kwa anayeomba nusura Yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek