Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 19 - النور - Page - Juz 18
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ ٱلۡفَٰحِشَةُ فِي ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ ﴾
[النور: 19]
﴿إن الذين يحبون أن تشيع الفاحشة في الذين آمنوا لهم عذاب أليم﴾ [النور: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa hakika,wale wanaopenda kuenea machafu kwa Waislamu, ya tuhuma za uzinifu au jambo lolote baya, watapata adhabu kali ulimwenguni, kwa kupigwa mboko, na mengineyo miongoni mwa mitihani ya kilimwengu, na watapata adhabu ya Motoni huko Akhera wakiwa hawakutubia. Na Mwenyezi Mungu, peke Yake, Ndiye Anayejua urongo wao na Ndiye Anayeyajua maslahi ya waja wake na mwisho wa mambo , na nyinyi hamyajui hayo |