Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 21 - النور - Page - Juz 18
﴿۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ وَمَن يَتَّبِعۡ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَإِنَّهُۥ يَأۡمُرُ بِٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۚ وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ مَا زَكَىٰ مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ أَبَدٗا وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يُزَكِّي مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ ﴾
[النور: 21]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا تتبعوا خطوات الشيطان ومن يتبع خطوات الشيطان فإنه﴾ [النور: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazitekeleza sheria Zake, msiziandame njia za Shetani. Na yoyote anayefuata njia za Shetani, basi (huyo Shetani) anamuamrisha vitendo viovu na vichafu. Na lau si wema wa Mwenyezi Mungu kwa Waumini na rehema zake kwao, hanagalitakasika yoyote katika wao kabisa na uchafu wa madhambi yake. Lakini Mwenyezi Mungu, kwa wema wake, Anamtakasa Anayemtaka. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia maneno yenu , ni Mjuzi wa nia zenu na matendo yenu |