Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 22 - النور - Page - Juz 18
﴿وَلَا يَأۡتَلِ أُوْلُواْ ٱلۡفَضۡلِ مِنكُمۡ وَٱلسَّعَةِ أَن يُؤۡتُوٓاْ أُوْلِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينَ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ وَلۡيَعۡفُواْ وَلۡيَصۡفَحُوٓاْۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٌ ﴾
[النور: 22]
﴿ولا يأتل أولو الفضل منكم والسعة أن يؤتوا أولي القربى والمساكين والمهاجرين﴾ [النور: 22]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala wasiape watu wema katika Dini na wakunjufu wa mali kuacha kuwaunga watu wao wa karibu wasiokuwa na kitu na wahitaji na wageni waliogura makwao na kuwanyima matumizi kwa sababu kuna kosa walilifanya. Basi na wayasamehe maovu yao wala wasiwatese. Kwani nyinyi hamupendi Mwenyezi Mungu Awasamehe? Basi wasameheni. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwasamehe waja Wake, ni Mwenye huruma kwao. Katika haya pana mahimizo juu ya kusamehe na kusahau kabisa, hata kama mtu atatendewa uovu |