×

Na wajizuilie na machafu wale wasio pata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu 24:33 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nur ⮕ (24:33) ayat 33 in Swahili

24:33 Surah An-Nur ayat 33 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 33 - النور - Page - Juz 18

﴿وَلۡيَسۡتَعۡفِفِ ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغۡنِيَهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۗ وَٱلَّذِينَ يَبۡتَغُونَ ٱلۡكِتَٰبَ مِمَّا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡ فَكَاتِبُوهُمۡ إِنۡ عَلِمۡتُمۡ فِيهِمۡ خَيۡرٗاۖ وَءَاتُوهُم مِّن مَّالِ ٱللَّهِ ٱلَّذِيٓ ءَاتَىٰكُمۡۚ وَلَا تُكۡرِهُواْ فَتَيَٰتِكُمۡ عَلَى ٱلۡبِغَآءِ إِنۡ أَرَدۡنَ تَحَصُّنٗا لِّتَبۡتَغُواْ عَرَضَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَمَن يُكۡرِههُّنَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ مِنۢ بَعۡدِ إِكۡرَٰهِهِنَّ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[النور: 33]

Na wajizuilie na machafu wale wasio pata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhila yake. Na wanao taka kuandikiwa uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni. Wala msiwashurutishe vijakazi vyenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta pato la maisha ya dunia, ilhali wao wanataka kujihishimu. Na atakaye walazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وليستعفف الذين لا يجدون نكاحا حتى يغنيهم الله من فضله والذين يبتغون, باللغة السواحيلية

﴿وليستعفف الذين لا يجدون نكاحا حتى يغنيهم الله من فضله والذين يبتغون﴾ [النور: 33]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na wale wasiokuwa na uwezo wa kuoa kwa ufukara wao au kwa jambo lingine, basi na wajizoeze uvumilivu wa kutoyafanya Aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, mpaka Mwenyezi Mungu Awatosheleze kwa wema Wake na Awasahilishie kuoa. Na wale wanaotaka kujikomboa na utumwa na ujakazi kwa kufanya mkataba na mabwana zao kwa kutoa kiasi maalumu cha pesa wawapatie, basi ni juu ya hao wamiliki wao waandikiane mapatano na wao kwa hilo, iwapo watajua kuwa kuna wema ndani yao ya uongofu, uwezo wa kujitafutia pesa na wema wa Dini. Na ni juu yao, hao wamiliki, wawape pesa, hao watumwa wao, au wawasamehe sehemu ya pesa walioandikiana. Na haifai kwenu kuwalazimisha wajakazi wenu kufanya uzinifu kwa lengo la kutaka kupata pesa. Na vipi litapatikana kwenu hilo na huku wao wenyewe wanataka kujilinda na uchafu huo, na nyinyi mnawakatalia hilo? Katika haya, pana kuonesha ubaya wa kitendo kiovu walichokifanya. Na yoyote mwenye kuwalazimisha wao kufanya uzinifu, basi Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, baada ya kuwalazimisha wao, ni mwenye kuwasamehe (hao waliolazimishwa) na kuwaonea huruma, na dhambi ni kwa yule Aliyewalazimisha
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek