Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 32 - النور - Page - Juz 18
﴿وَأَنكِحُواْ ٱلۡأَيَٰمَىٰ مِنكُمۡ وَٱلصَّٰلِحِينَ مِنۡ عِبَادِكُمۡ وَإِمَآئِكُمۡۚ إِن يَكُونُواْ فُقَرَآءَ يُغۡنِهِمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ ﴾
[النور: 32]
﴿وأنكحوا الأيامى منكم والصالحين من عبادكم وإمائكم إن يكونوا فقراء يغنهم الله﴾ [النور: 32]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na waozeni, enyi Waumini, wanaume wasiokuwa na wake na wanawake wasiokuwa na waume, miongoni mwa waungwana na walio wema kati ya watumwa wenu na wajakazi wenu. Iwapo anayetaka kuoa kwa kujihifadhi ni masikini mwenye uhitaji, Mwenyezi Mungu Atamtosheleza kutokana na ukunjufu wa riziki Yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu, ni Mwingi wa kheri, ni Mkuu wa fadhila na ni Mjuzi mno wa nyenendo za waja Wake |