Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 50 - النور - Page - Juz 18
﴿أَفِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَمِ ٱرۡتَابُوٓاْ أَمۡ يَخَافُونَ أَن يَحِيفَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَرَسُولُهُۥۚ بَلۡ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ ﴾
[النور: 50]
﴿أفي قلوبهم مرض أم ارتابوا أم يخافون أن يحيف الله عليهم ورسوله﴾ [النور: 50]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, sababu ya kupa mgongo kwao ni ule ugonjwa wa unafiki ulio ndani ya nyoyo zao au wanaushuku unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie? Au sababu ni kuchelea kwao isije ikawa hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni ya maonevu? Ukweli ni kwamba wao hawaogopei maonevu, isipokuwa kiini hasa ni kwamba wao wenyewe ndio madhalimu walio waovu |