Quran with Swahili translation - Surah Al-Furqan ayat 20 - الفُرقَان - Page - Juz 18
﴿وَمَآ أَرۡسَلۡنَا قَبۡلَكَ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ إِلَّآ إِنَّهُمۡ لَيَأۡكُلُونَ ٱلطَّعَامَ وَيَمۡشُونَ فِي ٱلۡأَسۡوَاقِۗ وَجَعَلۡنَا بَعۡضَكُمۡ لِبَعۡضٖ فِتۡنَةً أَتَصۡبِرُونَۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرٗا ﴾
[الفُرقَان: 20]
﴿وما أرسلنا قبلك من المرسلين إلا إنهم ليأكلون الطعام ويمشون في الأسواق﴾ [الفُرقَان: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hatukumtumiliza yoyote kabla yako, ewe Mtume, miongoni mwa Mitume wetu, isipokuwa walikuwa binadamu, wanaokula chakula na wanaoenda sokoni. Na tumewafanya baadhi yenu, enyi watu, ni maonjo na mtihani kwa wengine, kwa uongofu na upotevu, utajiri na umasikini, uzima na ugonjwa. Basi je, mtavumilia msimame imara juu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewalazimisha nayo na mumshukuru ili Mola wenu awape malipo mema au hamtavumilia mustahili kuteswa? Na Mola wako, ewe Mtume, Anamuona anayepapatika au anayevumilia, na anayekanusha au anayeshukuru |