Quran with Swahili translation - Surah Al-Furqan ayat 3 - الفُرقَان - Page - Juz 18
﴿وَٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةٗ لَّا يَخۡلُقُونَ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ وَلَا يَمۡلِكُونَ لِأَنفُسِهِمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗا وَلَا يَمۡلِكُونَ مَوۡتٗا وَلَا حَيَوٰةٗ وَلَا نُشُورٗا ﴾
[الفُرقَان: 3]
﴿واتخذوا من دونه آلهة لا يخلقون شيئا وهم يخلقون ولا يملكون لأنفسهم﴾ [الفُرقَان: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na washirikina wa kiarabu walitengeneza waungu, wasiokuwa Mwenyezi Mungu. Waungu hao hawawezi kuumba chochote, na Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewaumba wao na wenye kuwaabudu, wala hawana uwezo wa kuzuia madhara wala kujiletea manufaa, wala hawawezi kukifisha kilicho hai wala kukihuisha kilichokufa au kumfufua yoyote, miongoni mwa wafu, akiwa hai kutoka kaburini mwake |