Quran with Swahili translation - Surah Al-Furqan ayat 59 - الفُرقَان - Page - Juz 19
﴿ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَسۡـَٔلۡ بِهِۦ خَبِيرٗا ﴾
[الفُرقَان: 59]
﴿الذي خلق السموات والأرض وما بينهما في ستة أيام ثم استوى على﴾ [الفُرقَان: 59]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Aliyeumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake kwa Siku sita, kisha akalingana juu ya '“Arsh - yaani Akawa juu na Akaangatika- kulingana kunakonasibiana na utisho Wake, Yeye Ndiye Mwingi wa rehema. Basi muulize, ewe Mtume, Mtambuzi kuhusu Yeye. Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Anajikusudia Mwenyewe Aliyetukuka, kwani Yeye Ndiye Anayejua sifa Zake, ukuu Wake na utukufu Wake. Na hakuna yoyote, katika binadamu, anayemjua zaidi Mwenyezi Mungu wala anayetambua habari Zake zaidi kuliko mja Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye |