Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 14 - النَّمل - Page - Juz 19
﴿وَجَحَدُواْ بِهَا وَٱسۡتَيۡقَنَتۡهَآ أَنفُسُهُمۡ ظُلۡمٗا وَعُلُوّٗاۚ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ ﴾
[النَّمل: 14]
﴿وجحدوا بها واستيقنتها أنفسهم ظلما وعلوا فانظر كيف كان عاقبة المفسدين﴾ [النَّمل: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na waliikanusha, Fir’awn na watu wake, miujiza tisa yenye kuonyesha wazi ukweli wa Mūsā katika unabii wake na ukweli wa ulinganizi wake, na walikanusha kwa ndimi zao kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu, na hali wana yakini nayo ndani ya nyoyo zao, kwa kuifanyia uadui haki na kuwa na kiburi cha kutoikubali. Basi angalia , ewe Mtume, ulikuwa vipi mwisho wa wale waliozikanusha aya za Mwenyezi Mungu na wakafanya uharibifu kwenye ardhi? Mwenyezi Mungu aliwazamisha baharini. Na katika hilo kuna mazingatio kwa anayezingatia |