×

Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. 27:40 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Naml ⮕ (27:40) ayat 40 in Swahili

27:40 Surah An-Naml ayat 40 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 40 - النَّمل - Page - Juz 19

﴿قَالَ ٱلَّذِي عِندَهُۥ عِلۡمٞ مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن يَرۡتَدَّ إِلَيۡكَ طَرۡفُكَۚ فَلَمَّا رَءَاهُ مُسۡتَقِرًّا عِندَهُۥ قَالَ هَٰذَا مِن فَضۡلِ رَبِّي لِيَبۡلُوَنِيٓ ءَأَشۡكُرُ أَمۡ أَكۡفُرُۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيّٞ كَرِيمٞ ﴾
[النَّمل: 40]

Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قال الذي عنده علم من الكتاب أنا آتيك به قبل أن يرتد, باللغة السواحيلية

﴿قال الذي عنده علم من الكتاب أنا آتيك به قبل أن يرتد﴾ [النَّمل: 40]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Akasema yule ambaye alikuwa na ujuzi kutoka kwenye Kitabu, «Mimi nitakuletea hiko kitanda kabla ya kupepesa macho yako yanapogeuka kuangalia kitu.» Sulaymān akamruhusu, naye akamuomba Mwenyezi Mungu na akakileta kitanda cha kifalme. Alipokiona Sulaymān kimehudhurishwa mbele yake na kimethibiti alisema, «Huu ni miongoni mwa wema wa Mola wangu Aliyeniumba na akaumba ulimwengu wote ili kunitahini mimi nitalishukuru hilo kwa kutambua neema Yake Aliyetukuka au nitakufuru kwa kuacha kushukuru? Na mwenye kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema Zake, nafuu ya hilo itamrudia yeye mwenyewe, na mwenye kukanusha neema na akaacha kushukuru, basi hakika Mola wangu Ametosheka Hahitajii shukrani yake, ni Karimu ambaye kheri Yake inamuenea hapa duniani mwenye kushukuru na mwenye kukufuru, kisha Atawahesabu huko Akhera na awalipe
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek