Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 83 - النَّمل - Page - Juz 20
﴿وَيَوۡمَ نَحۡشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ فَوۡجٗا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِـَٔايَٰتِنَا فَهُمۡ يُوزَعُونَ ﴾
[النَّمل: 83]
﴿ويوم نحشر من كل أمة فوجا ممن يكذب بآياتنا فهم يوزعون﴾ [النَّمل: 83]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na siku tutakayokusanya- Siku ya Ufufuzi- katika kila jamii, kundi la watu, miongoni mwa wale wanaozikanusha aya zetu na hoja zetu, watazuiliwa wa mwanzo wao wachanganywe na wa mwisho wao, wapate kukusanyika wote, kisha waongozwe hadi pale pa kuhesabiwa |