Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 38 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَأُ مَا عَلِمۡتُ لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرِي فَأَوۡقِدۡ لِي يَٰهَٰمَٰنُ عَلَى ٱلطِّينِ فَٱجۡعَل لِّي صَرۡحٗا لَّعَلِّيٓ أَطَّلِعُ إِلَىٰٓ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُۥ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ﴾
[القَصَص: 38]
﴿وقال فرعون ياأيها الملأ ما علمت لكم من إله غيري فأوقد لي﴾ [القَصَص: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Fir’awn akasema kuwaambia watukufu wa watu wake, «Enyi viongozi! Mimi sijui kwamba nyinyi muna mola isipokuwa mimi anayestahiki kuabudiwa. Basi, ewe Hāmān! Niwashie moto juu ya udongo mpaka ushikane, na unijengee jengo lenye urefu wa kuelekea juu, kwani huenda nikamchungulia muabudiwa wa Mūsā ambaye yeye anamuabudu na anawaita watu wamuabudu. Na mimi ninadhani kuwa yeye ni miongoni mwa warongo katika hayo anayoyasema.» |