Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 41 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَئِمَّةٗ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلنَّارِۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴾
[القَصَص: 41]
﴿وجعلناهم أئمة يدعون إلى النار ويوم القيامة لا ينصرون﴾ [القَصَص: 41]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tumemfanya Fir’awn na watu wake ni wenye kuongoza kwenye njia ya motoni, wakifuatwa na watu wa ukafiri na uasi. Na Siku ya Kiyama hawataokolewa. Hiyo ni kwa sababu ya ukafiri wao na kuwakanusha kwao Mitume wa Mola wao na kuendelea kwao kufanya hivyo |