Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 57 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَقَالُوٓاْ إِن نَّتَّبِعِ ٱلۡهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفۡ مِنۡ أَرۡضِنَآۚ أَوَلَمۡ نُمَكِّن لَّهُمۡ حَرَمًا ءَامِنٗا يُجۡبَىٰٓ إِلَيۡهِ ثَمَرَٰتُ كُلِّ شَيۡءٖ رِّزۡقٗا مِّن لَّدُنَّا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[القَصَص: 57]
﴿وقالوا إن نتبع الهدى معك نتخطف من أرضنا أو لم نمكن لهم﴾ [القَصَص: 57]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na makafiri wa Makkah wanasema, «Tukiifuata haki uliyotuletea na tukajiepusha na wategemewa na waungu, tutanyakuliwa kutoka kwenye ardhi yetu kwa kuuawa na kutekwa na kuporwa mali.» Kwani hatukuwafanya wao wamakinifu ndani ya mji wa amani, ambao ndani yake tumeharamisha umwagaji damu na ambao yanaletwa huko matunda ya kila aina yakiwa ni riziki kutoka kwetu? Lakini wengi wa hawa washirikina hawajui kadiri ya neema hizi kwao, wakapata kumshukuru Aliyewaneemesha wao kwazo na wakamtii |