Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 61 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿أَفَمَن وَعَدۡنَٰهُ وَعۡدًا حَسَنٗا فَهُوَ لَٰقِيهِ كَمَن مَّتَّعۡنَٰهُ مَتَٰعَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا ثُمَّ هُوَ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ مِنَ ٱلۡمُحۡضَرِينَ ﴾
[القَصَص: 61]
﴿أفمن وعدناه وعدا حسنا فهو لاقيه كمن متعناه متاع الحياة الدنيا ثم﴾ [القَصَص: 61]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, yule tuliyomuahidi Pepo, miongoni mwa viumbe wetu, kwa sababu ya kututii, akawa ni mwenye kupata alichoahidiwa na ni mwenye kukifikia, ni kama yule tuliyempa, katika uhai wa kilimwengu, starehe zake, naye akastarehe nazo na akaipa mbele ladha ya karibu kuliko ile ya baadaye, kisha yeye akawa ni mwenye kuhudhurishwa Siku ya Kiyama ili ahesabiwe na alipwe? Makundi mawili haya hayalingani. Basi mwenye akili ajichagulie nafsi yake kile kilicho bora kuchagua, nacho ni kule kumtii Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi Zake |