Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 76 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿۞ إِنَّ قَٰرُونَ كَانَ مِن قَوۡمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيۡهِمۡۖ وَءَاتَيۡنَٰهُ مِنَ ٱلۡكُنُوزِ مَآ إِنَّ مَفَاتِحَهُۥ لَتَنُوٓأُ بِٱلۡعُصۡبَةِ أُوْلِي ٱلۡقُوَّةِ إِذۡ قَالَ لَهُۥ قَوۡمُهُۥ لَا تَفۡرَحۡۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَرِحِينَ ﴾
[القَصَص: 76]
﴿إن قارون كان من قوم موسى فبغى عليهم وآتيناه من الكنوز ما﴾ [القَصَص: 76]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Qārūn alikuwa ni miongoni mwa watu wa jamii ya Mūsā, rehema na amani zimshukiye, akakiuka mpaka wake katika kuwa na kiburi na ujabari juu yao. Na tulimpa Qārūn mahazina mengi ya mali, mpaka ikafikia kiwango cha kuwa funguo zake zinawaelemea idadi kubwa ya watu wenye nguvu kuzibeba. Walipomuambia watu wake, «Usifanye kiburi ukawa na gogi la furaha kwa mali uliyonayo. Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi kati ya waja wake wale wenye kiburi ambao hawamshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa kile Alichowapa |