Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 77 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَٱبۡتَغِ فِيمَآ ءَاتَىٰكَ ٱللَّهُ ٱلدَّارَ ٱلۡأٓخِرَةَۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ ٱلدُّنۡيَاۖ وَأَحۡسِن كَمَآ أَحۡسَنَ ٱللَّهُ إِلَيۡكَۖ وَلَا تَبۡغِ ٱلۡفَسَادَ فِي ٱلۡأَرۡضِۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُفۡسِدِينَ ﴾
[القَصَص: 77]
﴿وابتغ فيما آتاك الله الدار الآخرة ولا تنس نصيبك من الدنيا وأحسن﴾ [القَصَص: 77]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Na utafute, kwa mali Aliyokupa Mwenyezi Mungu, malipo mema ya Nyumba ya Akhera, kwa kufanyia mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu duniani, na usiache fungu lako la duniani la kustarehe humo kwa halali bila kupita kiasi, na uwafanyie watu hisani kwa kuwapa sadaka kama vile Mwenyezi Mungu Alivyokufanyia hisani kwa kukupa mali mengi haya, na usitafute kile Alichokiharamisha Mwenyezi Mungu cha kuwadhulumu watu wako, kwani hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi waharibifu, na Atawalipa kwa matendo yao mabaya.» |