Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 3 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَلَقَدۡ فَتَنَّا ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَلَيَعۡلَمَنَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَلَيَعۡلَمَنَّ ٱلۡكَٰذِبِينَ ﴾
[العَنكبُوت: 3]
﴿ولقد فتنا الذين من قبلهم فليعلمن الله الذين صدقوا وليعلمن الكاذبين﴾ [العَنكبُوت: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa hakika, tuliwajaribu wale waliokuwa kabla yao miongoni mwa ummah mbalimbali na tukawatahini kwa Mitume wetu tuliowatumiliza kwao. Basi hakika ni kwamba Mwenyezi Mungu Atawajua, ujuzi wa kujitokeza nje kwa viumbe, ukweli wa wale wakweli katika Imani yao na urongo wa warongo, ili Alipambanue kila kundi na lingine |