Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 31 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُوٓاْ إِنَّا مُهۡلِكُوٓاْ أَهۡلِ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةِۖ إِنَّ أَهۡلَهَا كَانُواْ ظَٰلِمِينَ ﴾
[العَنكبُوت: 31]
﴿ولما جاءت رسلنا إبراهيم بالبشرى قالوا إنا مهلكو أهل هذه القرية إن﴾ [العَنكبُوت: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Malaika walipomjia Ibrāhīm na habari ya furaha itokayo kwa Mwenyezi Mungu ya (kuzaliwa) Isḥāq, na nyuma ya Isḥāq ni mwanawe, Ya’qūb, walisema wale Malaika, «Sisi ni wenye kuwaangamiza watu wa kijiji cha watu wa Lūṭ, nacho ni Sadūm, kwa kuwa watu wake wamekuwa ni wenye kujidhulumu wenyewe kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.» |