Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 46 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿۞ وَلَا تُجَٰدِلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡۖ وَقُولُوٓاْ ءَامَنَّا بِٱلَّذِيٓ أُنزِلَ إِلَيۡنَا وَأُنزِلَ إِلَيۡكُمۡ وَإِلَٰهُنَا وَإِلَٰهُكُمۡ وَٰحِدٞ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 46]
﴿ولا تجادلوا أهل الكتاب إلا بالتي هي أحسن إلا الذين ظلموا منهم﴾ [العَنكبُوت: 46]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wala msijadiliane, enyi Waumini, na Mayahudi na Wanaswara isipokuwa kwa njia nzuri na maneno mazuri na kulingania kwenye haki kwa njia sahali yenye kupelekea kwenye lengo hilo, isipokuwa wale ambao wamekaa kando na haki wakafanya ushindani na kiburi na wakatangaza vita juu yenu, basi hao piganeni nao kwa upanga mpaka waamini au watoe jizia (kodi maalumu) kwa mkono na wao wakiwa katika hali ya unyonge. Na semeni, «Tumeiamini Qur’ani iliyoteremshwa kwetu, na tumeiamini Taurati na Injili ambazo mliteremshiwa, na Mola wetu na Mola wenu ni Mmoja Hana mshirika Wake katika uungu Wake, wala katika sifa Yake ya kuwa ni Mola, wala majina Yake na sifa Zake. Na sisi ni wenye kunyenyekea na kujifanya wanyonge Kwake kwa kumtii katika yale Aliyotuamrisha na Aliyotukataza |